Ule mpambano wa masumbwi jukwaani uliokuwa uwakitanishe mastaa Soulja Boy na Chris Brown unawezekana usifanyike.
Baada ya mpambano huo kutangazwa na mashabiki kungoja kwa hamu kubwa,upande wa timu ya rapa Soulja Boy umesema kuna dalili kubwa mpambano huo unaweza usifanyike kwa kile walichadi kwamba mpinzani wao Breezy kumhofia Soulja Boy na ndiyo maana mpaka kufikia jumapili Feb. 19 Brown alikuwa bado hajasaini mkataba wa mpambano huo.
Timu ya rapa Soulja Boy imeidi kujigamba na kusema huenda Breezy amepatwa na uoga baada ya kupata taarifa kwamba mpinzani wake Soulja Boy ameshinda mapambano mawili ya kimtaamtaa pale majaa walipotaka kumvaa.
Tuesday, February 21, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment