Peter Okoye aka Mr P ambaye ni mmoja wa wanaounda kundi mahiri la muziki la P-Square,asema ikitokea anapata mualiko wa kutumbuiza atatumbuiza nyimbo na za P-Square.
Peter Okoye aliyasema hayo pale alipokuwa akijibu sali la shabiki mmoja aliyetaka kujua kama ikiwa atakuwa na onyesho ataimba record za P-Square.
Hii ni kutokana na kile ambacho kinasemwa kugawanyika kwa kundi la ndugu mapacha P-Square baada ya kutokea mtafaruku baina yao na Peter Okoye, aka Mr P kusema anaanza kupokea booking za matamasha kama msanii solo.
Peter tayari amepost picha katika Instagram akipromote onyesho lake linalokuja la huko Dallas.
0 comments:
Post a Comment