Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Wednesday, May 21, 2014


Muimbaji wa muziki wa kizazi kipya mwenye uwezo wa sauti ya juu kabisa,Aboubakary Katwila almaarufu kama Q Chief ama Q Chilla,amesema amefurahishawa sana na mwenendo na jitihada za muimbaji wa muziki wa kizazi kipya Nassib Abdul maarufu kama Diambond Platnums,Q Chilla amesema anaamini mafanikio tuyaonayo ya  Diambond Platnums ni matunda ya kujituma na kuwekeza katika kazi ya muziki.
Q Chilla ameyasema hayo katika maongezi na mwandishi wa blogu hii na kuongeza kusema,Diamond kushiriki tuzo za BET  ni habari njema kwa watanzania,anamuombea ashinde ila hata asipochukua tuzo hiyo tayari ni mshindi tayari.
Diamond Platnums anashiriki tuzo za BET kwenye kipengele cha Best International Act: Africa,ambapo anashindana na wasanii wakali kama Davio wa Nigeria,Mafikizolo wa South Africa,Sarkodie wa Ghana,Tiwa Svage wa Nigeria na Toofan wa Togo.

0 comments:

Post a Comment