Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Tuesday, May 13, 2014

 
Vyombo mbalimbali vya habari na hata mitandao ya kijamii imepambwa na story ama vichwa vya habari visemavyo,Dada wa Beyonce,Solange Knowles amshambulia Jay Z katika lift.
Taarifa zidi zinasema tukio hilo la Jay Z kushambuliwa na shemeji yake lilitokea katika Met Gala after party wiki iliyopita Standard Hotel huko NYC.Katika sehemu ya video wanaonekana Jay Z,Beyonce na Solange wakiingia katika lifti nakisha kumuonyesha Solangeakimkaripia Jay na baadaye kumvamia na kumshambulia kwa ngumi,vibao,mateke na kisha kumpiga na pochi.Katika lifti hiyo anaonekana mtu kama baunsa ambaye alijaribu kumzuia Solange bila mafanikio huku akimuachia upenyo wa kumshambulia Jay Z mara tatu zaidi wakati Beyonce akiwa pembeni bila kuingilia.Wakati ugomvi ukiendelea anaonekana mlinzi huyo akibonyeza emergency stop switch ghorofa ya 12 ili ugomvi uwe siri.

Baada ya ugomvi huo walionekana Bey na Solange wakipanda gari moja na Jay Z kupandishwa kwa gari lingine.Tukio hilo linawaacha mafans duniani kote kujiuliza nini kimepelekea Solange kumshambulia Jay Z hotelini Standard Hotel,New York City on May 5.Mtandao mmoja umeandika:
Solange hapendezewi na tabia ya Jay Z kumendesha Beyonce.Beyonce huwa aongei japo jambo hilo humkera ila kupitia mdogo wake ambaye ni Solange ujumbe umefika na ndiyo maana hata katika video anaonekana Beyonce akiangalia tu.
JAY-Z-solange-fight-met-ball-6  beyonce-jay-z-solange-1-

0 comments:

Post a Comment