Mmoja wa waasisi wa mtandao wa kijamii wa Instagram, ameambia BBC kuwa sheria zake kuhusu picha za uchi hazimbagui mtu yeyote.
Kampuni hiyo imekosolewa vikali kwa kwa kuondoa picha za wanawake walio nusu uchi kwenye mtandao huo.Lakini Afisaa mkuu mtendaji wa
mtandao huo wa kijamii, Kevin Systrom, amesema kuwa sheria hizo
zinalenga kuhakikisha kuwa vijana na watu wazima wanaotumia mtandao huo
wako salama.
Masharti ya matumizi ya mtandao wenyewe,
yanasema: 'Mtu haruhusiwi kuweka picha za watu walio nusu uchi na picha
zenye mada ya ngono. ''
Matamshi yake yanakuja baada ya mwanawe muigizaji maarufu, Bruce
Willis, Scout Willis kuweka picha yake kwenye mtandao huo akiwa nusu
uchi bila kitu kifuani.
Muimbaji Rihanna, ambaye alikuwa na wafuasi milioni 1.3 aliunga mkono kampeini hiyo kabla ya kufunga akaunti yake.
0 comments:
Post a Comment