Bbc.co.uk/Swahili imeandika,Uchunguzi wa utafiti kutoka chuo kikuu cha Exeter nchini Uingereza, unapendekeza
kuwa idadi ya mbegu za uzazi za wanaume huathiriwa kwa kuweka simu za mkononi
kwenye mifuko ya suruale.
Uchunguzi huo uliochapishwa katika jarida la 'Environment International'
ulilaumu mnunurisho wa kielectromagnetiki kuwa chanzo kikuu.
Lilichanganua tafiti kumi tofauti kuonyesha ubora wa shahawa ikihusisha
wanaume 1,492.Hii ilijumuisha kupimwa kwa shahawa zilizowekwa wazi kwa
mnunurisho wa simu za rununu, kwa maabara na udadisi wa wanaume katika cliniki
za uzazi
Kiongozi wa uchunguzi huo Dkt.Fiona Mathews aliambia BBC kuwa kutokana na
uchunguzi huo,moja tu ndio ulionyesha uhusiano kati ya utumizi wa simu na
kudidimia kwa ubora wa shahawa.
"Nafikiri kwa mwanamume wa makamu hakuna haja ya kuingiwa na hofu,iwapo
unajua una uwezekano wa kuwa na shida ya kizazi basi itakuwa jambo la busara
kutoweka simu mfukoni ,pia kugeuza mtindo wako wa kula.
Alikubali kukosolewa na wana sayansi wengine huku akiunga mkono kuwa kuna
umuhimu wa kufanya uchunguzi zaidi.
Dkt,Mathews alimaliza kwa kusema"hili ni jambo la kusisimua lakini hatusemi
kwa uhakika kuwa kila anayebeba simu mfukoni atakuwa na shida ya kizazi."
Monday, June 16, 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment