Muigizaji maarufu wa Marekani Halle
Berry, ameghadhabishwa mno na hatua ya aliyekuwa mumewe juu ya
kumbadilisha mwanawe rangi ya ngozi pamoja na kuweka kemikali kwenye
nywele zake ili ziwe singa.
Muigizaji huyo alikasirishwa na jambo
hilo kwani mwanawe mwenye umri wa miaka sita Nahla Berry ambaye kawaida
anakuwa na nywele koto ameanza kubadilika.Hapo ndipo hasira zilimpanda Halle Beryy kiasi cha kumpeleka mahakamani babake mtoto huyo Gabriel Aubry waliyeachana naye mwaka 2010.
Berry alinukuliwa akisema,'' kila siku wasiwasi unanizidi kuhusu athari atakazopata mwanangu Nahla kisaikolojia na kimwili kwa kuwekewa kemikali kwa nywele. Pia ataathirika kimawazo kutokana na mwili wake kuanza kubadilishwa.''
Pamoja na taarifa yake Berry aliweka picha za mwanawe za kabla na sasa ili kuonyesha jinsi mwanawe alivyobadilishwa rangi yake ya mwili huku nywele zake zikiwekwa kemikali ili kuwa singa.
Nataka mahakama kumuamuri babake mtoto huyu Gabriel kukoma juhudi zake za kubadilisha mwonekano wa mtoto wetu na labda kumsababisha mtoto kuanza kujiuliza kwa nini rangi nyeusi ya ngozi yake sio nzuri au haifai.
Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani Jumatatu na wakili wa Berry ambaye hakufika mahakamani. Inaarifiwa jaji jaji aliamuru kwamba kuanzia sasa, babake Nahla lazima akome kumbadilisha mwonekeno wa mtoto.
Halle Berry na Aubry waliachana mwaka 2010 na jaji aliamua kuwa wote wawili hawana ruhusa ya kubadilisha sura na mwonekano wa mtoto wao kivyovyote.
0 comments:
Post a Comment