Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Saturday, March 21, 2015


Drake and Lil Wayne
Msanii wa muziki wa rap nchini Marekani,Lil Wayne katika kitabu alichoandika amesema alikuwa tayari kumshambulia msanii mwenza ambaye pia ni rafiki yake,Drake kwa kile alichosema kwamba rafiki yake huyo alimwendea kinyume na mpenzi wake.Mtandao wa kidaku wa TMZ wa nchini Marekani,ulipata taarifa ya mapendekezo ya kitabu hicho ambayo yametumwa kwa wachapishaji kadhaa.
Wayne anadai kwamba wakati alipokuwa akihudumia kifungo chake jela katika kisiwa cha Rakers kwa kumiliki bunduki bila kibali,inadaiwa kuwa Drake alimtembelea na kukiri mbele yake kwamba ali lala na mpenziwe.Lil Wayne alisema :Hiki ni kitendo ambacho mwanamume ambaye yuko jela hapendi kusikia kwa sababu ni mungu anayejua ni nini ningelifanya iwapo ningekuwa nje.
Wayne alikiri katika mapendekezo hayo kwamba yeye na mpenziwe walikuwa wakigombana sana ndipo Drake akamwambia kwamba alilala naye.Hatahivyo Wayne anasema kuwa mwanamke huyo alimwambia kwamba alifanya mapenzi na Drake siku moja kabla ya kukutana na Wayne.

0 comments:

Post a Comment