Muimbaji Ariana Grande 21, na rapa Big Sean 27, walitangaza kuwa katika mahusiano ya kimapenzi mwezi August 2014. Alikuwa ni Ariana aliyedhihirisha mahusiano hayo mwezi October alipofaniwa mahojiano na mwandishi wa gazeti la U.K. Telegraph Magazine,kwa kusema rappa Big Sean is one of the most amazing men in the whole world.
Wawili hao wametangaza kuvunja mahusiano yao ya kimapenzi kupitia wawakilishi wao na kutangaza kwamba watabakia kuwa marafiki wa karibu na kuomba vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuheshimu makubalianao yao hao.
Kwa mujibu wa jarida la Us Weekly, inasemekana wawili hao wamefikia uamuzi huo baada ya kutokea kutokuelewana katika maswala ya ratiba na mipango ya kazi haswa ratiba za ziara za muziki.
0 comments:
Post a Comment