Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Thursday, April 30, 2015


Sean “Diddy” Combs yupo tayari kuingia tena barabarani kwaajili ya matamasha.Bosi huyo wa The Bad Boy  ametangaza mpango wake wa kufanya ziara ya kuizunguka duni (world tour).
Huku akifanya kampeni za kutangaza vinywaji vya DeLeón Tequila,leo siku ya alhamis,diddy alitangaza mpango wake huo alipokuwa akihojiwa katika kipindi cha televisheni cha “The Ellen DeGeneres Show.”
Diddy mwenye umri wa miaka 45 alisema:“I’m gonna go and do a world tour,” “I’m not gonna hit a lot of places, but the places that I am gonna hit, it’s important for me because it’s probably my last time touring.”
Akimaanisha hatotembea na kufanya maonyesho sehemu zote za dunia bali atachagua sehemu alizozipa uzito kwani inawezekana ikawa ni ziara yake ya mwisho kimuziki.
 Mara ya mwisho Diddy kufanya ziara ya muziki alifanya na Dirty Money katika miji 20,ziara waliyoipa jina “Coming Home” mwaka 2011 walipokuwa wakifanya kampeni ya kuitangaza albamu yao ya Last Train to Paris.
Sambamba na ziara hiyo Diddy amesema yupo jikoni kupika albamu mpya itayokwenda kwa jina la MMM na anatimu ya maproducer kama Kanye West, The Weeknd, The Lox, Pusha T, A$AP Ferg, na Cassie.

0 comments:

Post a Comment