Sean “Diddy” Combs yupo tayari kuingia tena barabarani kwaajili ya
matamasha.Bosi huyo wa The Bad Boy ametangaza mpango wake wa kufanya
ziara ya kuizunguka duni (world tour).
Huku akifanya kampeni za kutangaza vinywaji vya DeLeón Tequila,leo
siku ya alhamis,diddy alitangaza mpango wake huo alipokuwa akihojiwa
katika kipindi cha televisheni cha “The Ellen DeGeneres Show.”
Diddy mwenye umri wa miaka 45 alisema:“I’m gonna go and do a world tour,” “I’m not gonna hit a
lot of places, but the places that I am gonna hit, it’s important for me
because it’s probably my last time touring.”
Akimaanisha
hatotembea na kufanya maonyesho sehemu zote za dunia bali atachagua
sehemu alizozipa uzito kwani inawezekana ikawa ni ziara yake ya mwisho
kimuziki.
Mara ya mwisho Diddy kufanya ziara ya muziki
alifanya na Dirty Money katika miji 20,ziara waliyoipa jina “Coming
Home” mwaka 2011 walipokuwa wakifanya kampeni ya kuitangaza albamu yao
ya Last Train to Paris.
Sambamba na ziara hiyo Diddy amesema yupo jikoni kupika albamu mpya itayokwenda kwa jina la MMM na anatimu ya maproducer kama Kanye West, The Weeknd, The Lox, Pusha T, A$AP Ferg, na Cassie.
Thursday, April 30, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment