Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Monday, April 20, 2015


 
Hit maker wa ngoma ya hiphop iliyotingisha,Special Delivery,G-Dep kwasasa yupo gerezani akitumikia kifungo cha miaka 15 kufuatia kujipeleke mwenyewe mikononi mwa sheria kufuatia tukio la kupora na kusababisha mauaji alilolifanya mwaka 1993. 
Rapa G-Dep ambaye jina lake kamili ni Trevell Coleman, alikiri mwenyewe mahakamani kwamba yeye ndiye mhusika wa tukio mwaka 1993 la kupora na kuua japo hapo awali alijetetea na kuonekana hana makosa.
G Deep hapo hawali alishiriki katika albamu ya rapa mwenzake Black Rob, Life Story na baadaye akaachia albamu yake ya kwanza mwaka 2001. Taarifa zaidi zinasema rappa G Deep alifikia uamuzi wa kutubu na kusema ukweli japo mahakama ilishindwa kumkuta na hatia,baada ya kuongea na kukubaliana na watu wake wa karibu kikazi na familia pale alipowaambia ameamua kutubu ili asamehewe na Mungu na ilikuwa ikimsumbua kila mara katika maisha yake.Rappa G Deep alikiri kosa mahakamani na kuomba radhi kwa familia ya waliompoteza mpendwa wao.
Alivyoachiwa kwa muda wiki iliyopita ahudhurie mazishi ya baba yake,alikuata na mke na watoto wake wawili ambao aikuwa hajawaona kwa takribani miaka 4.
Rappa G Deep anakmbukwa sana kwa kazi yake "Special Delivery" ambayo ni singo aliyoitoa akiwa na Bad Boy kutoka katika albamu "Child of the Ghetto".


0 comments:

Post a Comment