Beyoncé anautumia u star wake vema.Malkia wa mitindo ya R&B ambaye pia ni mke wa m babe wa mitindo ya hiphop duniani,Jay -Z,Beyonce,ametumia vema vema nguvu ya umaarufu aliobarikiwa baada ya kutembelea hospitali maalumu ya watoto nchini Haiti,Saint Damien Pediatric
Hospital,kama sehemu ya mipango ya umoja wa mataifa katika shughuli za kujitolea za kibinadamu.
Beyonce akiwa nchini Haiti ambako ni nyumbani kwa mastaa kama Wyclf Jean,Prass,Jason Derul
alikutana na madaktari,watoto wagonjwa wa kansa na magonjwa mengineyo,watoto waliolazwa hospitalinihapo na hata kutembelea sehemu muhimu za hospitali hiyo kama intensive care unit(ICU).
Taarifa zaidi zinasema Beyonce alipeleka matumaini ya kuifungua tena hospitali hiyo maalumu kwaajili ya watoto wanaosumbuliwa na magonjwa sugu huko Haiti,baada ya kuelekea kufungwa kufuatia hali ya ukata uliokuwa ukiikabili.Beyonce ametunisha mfuko wa kuisadia hospitali hiyo kwa kuuza Tshirt zake zilizoandikwa “BeyGOOD” ambapo mauzo yote ya Tshit hizo yanaingia katika mfuko wa haspitali hiyo ya Saint Damien Pediatric Hospital.
Wednesday, June 10, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment