Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Friday, March 18, 2016

 Rihanna
Akiwa na zaidi ya muongo mmoja tu katika sanaa ya muziki na mitindo,Rihanna amezidi kuwa nyota inayong'ara siku baada ya siku.
Jarida la habari za kiburudani la marekani la Vogue limemtunuku pop star huyo kwa kumpatia heshima ya kupamba kasha lake la ukurasa wa mbele kwa picha yake kwaajili ya toleo la mwezi April 2016.
Katika sehemu ya habari ndani ya jarida hilo Rihanna ameongelea kuhusu albamu yake aliyoiachia mwezi February, ANTI na mitindo kama balozi wa Puma fashion line.

ANTI ni albamu yake aliyoitoa baada ya albamu yake ya mwisho Unapologetic,miaka 4 iliyopita na single, "Work" aliomshirikisha Drake,inafanya vema zaidi na imeshika No. 1 katika chati za Billboard's Hot 100
Rihanna pia alimuongelea na kumpa sifa rapa Drake kwa kusenma:
"Everything he does is so amazing,"

Rihanna na Drake wamekuwa katika mahusiano mazuri tofauti na ukilinganisha mahusiano kati ya Drake na Beyonce ambao haionyeshi kupatana huku wengi wakisema mengi na hata kuhusiha minong'ono kuhusu Jay Z kumzunguka Beyonce na kutoka na Rihanna.

0 comments:

Post a Comment