Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Monday, April 25, 2016

Mike Windle/Al Bello. Getty Images (2)
Albamu mpya ya Beyonce "LEMONADE" ambayo kwasasa inapatikana kama exclusive katika mtandao wa TIDAL baada ya kuwa premiered HBO juzi(April 23),exclusivity yake iliisha jana (April 24) kama ilivyoandikwa katika magazeti ya  New York Times hivyo albamu ya Beyonce, LEMONADE itakuwa inapatikana na katika mtandaowa iTunes.
LEMONADE ni albamu mpya iliyotoka kwa kushtukiza na ndani yake wameshirikishwa wakali wachacha akiwamo Kendrick Lamar na The Weeknd na kazi ya kuipika kufanywa na Diplo, Just Blaze na Hit-Boy .

Albamu hiyo ya Beyonce imekuja na kuzua maneno mengi huku zaidi yanayosemwa ni kwamba albamu hyo imebeba nyimbo nyingi kama madongo kwa mumewe ambaye ni Jay Z kuhusu kumchepuka.

Katika albamu hiyo mpya ya Beyonce "LEMONADE" kuna nimbo na mistari yake imepelekea wengi kutafsiri kuwa ni ma dongo,mfano katika wimbo  "Sorry,"   Beyonce  ameimba
"He only want me when I'm not there/ He better call Becky with the good hair."
Mistari katika wimbo huo inaonyesha kumlenga Rachel Roy ambaye alikuwa mke wa Dame Dash', na kilichopelekea watu kuamini zaidi ni pale Rache Roy alipoandika katika akaunti yake ya Twitter  (April 24) kwamba yeye ndiye ametajwa katika wimbo huo kwani Beyonce huwa anamshuku,ndipo alipoongezea kuandika:

"I respect love, marriages, families and strength,""What shouldn't be tolerated by anyone, no matter what, is bullying, of any kind."
Kingine kilichotajwa zaidi ni kuhusu neno "good hair" and "Becky." ambapo Rachel Roy katika instagram yake ameweka picha na kuandika ''Goog Hair don't care.Rachel Roy ametajwa kuwa ndiye chanzo cha ugomvi uliopelekea Jay Z kushambuliwa na shemeji yake ,Solanje katika lifti mwaka 2014, na siyo Rihanna kama ilivyokuwa ikitajwa hawali.

0 comments:

Post a Comment