Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Thursday, April 14, 2016

Tokeo la picha la dr dre and eve

Eve anafahamika sana kama mwana Ruff Ryders kwa takribani miongo miwili katika music industry. Eve ambaye hivi karibuni tutamuona katika the Barbershop: The Next Cut actress ameongelea safari yake katika muziki na changamoto kadhaa alizokutana nazo.
Akiwa na miaka 17 Eve amesema alikuwa na washikaji zake wakina "Mike Lynn ambao aliishi nao kama ma homeboy managers kwani walikuwa wanafahamu ana kipaji nao wana connection.Walikuwa wakimpa moyo na walikuwa wakimpatia sehemu ya mazoezi na vifaa.
Siku moja jamaa walimpigia Dre na kumwambia habari zake ndipo alipopata nafasi ya kurap kumsikilizisha Dr.Dre ambaye kwa namna moja alimkubali hivyo wakaanda wakutane,walipokutana tu cha kwanza alimuuliza kwanini unarap,kwanini upo na wavuta bangi wakubwa? kama upo tayari tusaini hakikisha unaacha bangi na unaachna na kampani ile,Eve akasema yeye huchill nao tu wale ila hatumii,haikuwa rahisi mpaka pale Dre alipojiridhisha ndipo alipomsaini Aftermath Entertainment.
Eve,hakutoa kazi yeyote na wala hakudumu muda mrefu ndani ya Aftermath Entertainment,akamwagwa kwa sababu ambazo hajaziweka wazi ndipi baadaye akapata nyumbani kupya, Ruff Ryders,alipofanya kazi na wakali DMX na Swizz Beatz na kufanikiwa kutoa albamu mbili kali na zenye mafanikio makubwa.
Eve amesema katika vitu hatovisahau ni pale kabla hajachukuliwa na Ruff Ryders alikutana na Mike Tyson na kupigwa bonge moja la mkwara yaani zile kama ntakuvunjavunja na ntakuua bila kusema nini kilikuwa chanzo.

0 comments:

Post a Comment