Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Friday, April 8, 2016



Huzuni umeghubika nchi ya Indonesia baada ya muimbaji maarufu nchini humo Irma Bule, aliyekuwa akitumbuiza kuanguka na kufariki dunia jukwaani
bi Bule aliumwa na nyoka dakika 45 kabla ya kuanza kutumbuiza katika ''shoo yake'' iliyokuwa magharibi mwa Indonesia.
Vyanzo vinaripoti  vinaripoti kuwa muimbaji huyo nyota alimkanyaga kimakosa nyoka huyo ambaye alikuwa sehemu ya ''shoo'' yake na kwa bahati mbaya nyoka huyo akamuuma kwenye paja.
Japo nyoka huyo alikuwa ameng'olewa meno yakelakini aliweza kum'gata na kuingiza sumu ndani ya damu yake.
Waliokuwapo eneo la tukio wanasema bi Bule alipewa dawa ya kutuliza makali ya sumu lakini akakataa akidhania kuwa nyoka yule hakumdhuru.
Bule aliendelea na onyesho hilo akiwatumbuiza mashabiki wake hadi pale alipoanza kutapika jukwani ndipo washirika wake wakang'amua hali haikuwa nzuri.
Mara akaanza kutetemeka na kuzirai.
Walipomkimbiza hospitalini daktari aliwaambia kuwa alikuwa ameshakata roho yake.

0 comments:

Post a Comment