Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Friday, April 8, 2016

 ____0182 2 2
April 8,wahusika wa kituo cha radio cha HOT 97 walitangaza orodha ya wasanii wakali watakaotumbuiza jukwaa kuu katika tamasha kubwa la muziki wa Hiphop linalofanyika kila mwaka linalofahamika kwa jina la Summer Jam concert ambalo litafanyika katika uwanja wa MetLife Stadium huko New Jersey,wasanii  hao ni Big Sean, Pusha T. & G.O.O.D Music, DJ Khaled & Friends , A$AP Rocky & A$AP Ferg.

Wengine waliotajwa kushambulia jukwaa ni sambamba na Bryson Tiller, Young Thug, Tinashe, Kid Ink na wengine watatangazwa siku za baadaye.

Kabla ya hapo watangazaji wa kipindi cha Ebro in the Morning ,Laura Stylez & Rosenberg walitangaza orodha ya wasanii watakaotumbuiza katika jukwaa la Festival ni sambamba na Chance the Rapper, Tory Lanez, Curren$y, Desiigner, Post Malone, Justine Skye, Dave East, Dougie F na Rotimi!
The festival stage performances itafanyika katika eneo la maegesho ya magari la uwanja huo wakati wa mchana kabla ya tamasha lenyewe usiku.
Tamasha la Hot 97 Summer Jam litafanyika MetLife Stadium siku ya jumapili , June 5.Tiketi zinaanza kuuzwa kuanzia , April 9 kupitia mtanda maalumu wa Ticketmaster.com,

0 comments:

Post a Comment