Justin Bieber amefunguliwa mashitaka ya kutakiwa kulipa dola 100,000 kwa madai kwamba alivunja simu.
Nyota
huyo ameingia matatani na kufungliwa mshtaka kwa kosa la kuivunja simu ya Robert Earl Morgan aliyekuwa akijaribu kumrekodi alipokuwa akinywa pombeKIsa hicxho kilitokea
katika kilabu ya Cle mjini Texas mwezi uliopita.Mtandao wa TMZ,umesema Justin Bieber alikasirishwa na kuchukua simu yake na kuivunja.
Thamani ya iPhone haifiki dola 100,000.
Lakini ameshtakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha kwa sababu simu hiyo ilikuwa na picha ambazo haziwezi kupatikana tena,ikiwemo picha za sherehe ya miaka 100 ya kuzaliwa kwa bibi yake.
Morgan pia anadai kwamba alipoteza idad kubwa ya nambari zake za mawasiliano ya biashara.
Bieber bado hajatoa tamko lolote kuhusu madai hayo.
Kisa hicho kinaaminika kufanyika jioni ambayo Bieber alionekana kumchoma na sigara Post Malone,ambay amekuwa akimsaidia katika ziara yake ya duniani.
Katika habari nyingine Justin Bieber alijaza watu mtaani na kusababisha foleni kubwa kuuatia kufungua duka la kuuza bidhaa zake haza mavazi yenye maaishi na picha zake.
Duka hilo la Biebs linafunguliwa kwa siku mbili tu yaani may 4 na 5 lipo katika mtaa wa Mercer Street ambapo imetajwa kuwa sambamba na bidhaa na mavazi yake pia atauza bidhaa zinazopromote ziara yake ya muziki ya Purpose tour.
0 comments:
Post a Comment