Nyota mpya kuwekwa mwakani katika sehemu maarufu duniani ya Hollywood Walk of Fame .
Wahusika na uwekaji wa nyota hizo za heshima,The Hollywood Chamber of Commerce and Walk of Fame wametangaza kuongeza nyota maka 2017,kwa masta Ice Cube, John Legend, na New Edition .
Hollywood Walk of Fame ni njia ya miguu iliopo mjini Hollywood Boulevard na Vine Street huko Hollywood, Los Angeles, California, Marekani,
ambayo hutumiwa kama sehemu ya maonyesho ya burudani. Imetiwa zaidi ya
nyota yenye-pembe tano 2,000 ikiwa na majina sio ya binadamu mashuhuri
peke yake bali hata yale ya wahusika wa katuni pia wamepewa nyota kwenye
Hollywood kwa mchango wao katika tasnia ya burudani.
Nyota za kwanza
zilitolewa mnamo mwezi wa Septemba katika mwaka wa 1958 na kuwekwa
kwenye njia ya miguu kwenye kona ya kaskazini mwa Hollywood Blvd. na Highland Ave.
Sambamba na mastaa Ice Cube, John Legend, na New Edition pia wametajwa *NSYNC, Clarence Avant, na late Selena.
Upande wa filamu wametajwa Amy Adams, Jason Bateman, Goldie Hawn,
Dwayne Johnson, Chris Pratt, Brett Ratner, Ryan Reynolds, George A.
Romero, Mark Ruffalo,na Rita Wilson.
Television stars ni Tyra Banks, Andre
Braugher, Ken Corday, Lee Daniels, Hugh Laurie, Eva Longoria, Wolfgang
Puck, Keri Russell, Haim Saban, George Segal, Sarah Silverman,na
Jeffrey Tambor.
Pia wapo mastaa upande wa radio ambao wote kwa ujumla watasimikiwa nyota zao katika sherehe maalumu ya usimikaji mwaka 2017 .
Hollywood Chamber of Commerce walianzisha mradi huo kama kivutio cha watalii ambao watatembelea Hollywood kuona nyota za wasanii wanaowapenda, directors , producers nk.
Wednesday, June 29, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment