Kufuatia tukio la kuingia matatani na vyombo vya sheria huko West Indies Island katika tamasha la St. Kitts festival baada ya kutumbuiza jukwaani kwa wimbo wenye lugha chafu,s Curtis Jackson aka 50 Cent ameripotiwa kulipa faini na sasa yupo njiani kurejea Marekani.
Rappa 50 Cent alijikuta mikononi mwa polisi  katia tamasha la  2016 St. Kitts Music Festival (June 25)  baada ya kumaliza kutumbuiza katika onyesho na kushuka jukwaani na kutajiwa kosa lake kuwa ni kuimba toleo chafu la hit yake ya  2003, "P.I.M.P." kosa ambalo upande wa wanachama wa G-Unit umesema wakulaumiwa ni DJ kwa kukosa kuwa na clean version ya wimbo huo P.I.M.P
Ifahamie kwamba 50 siye wa kwanza kukutana na matatizo kama hayo ,2003,rapa DMX alikutwa na mkasa kama huo katika tamasha kama hilo la St. Kitts Music Festival na akalipishwa faini.