Ja Rule na DMX wamekuwa matatizoni kisheria mara kwa mara kitu ambacho tunaweza amini kimewaharibia hata uwepo na uwezo wao katika sanaa hiyo.Mwezi July mwaka 2011, Ja Rule alifungwa miezi
28 jela kwa makosa ya kukwepa kulipa kodi,mwezi July mwaka 2007alikamatwa kwa makosa ya kumiliki silaha kinyume cha sheria na kukutwa na madawa ya kulevya.DMX naye ameshatumikia kifungo mara kwa mara kwa makosa kama hayo.
Wawili hao wameshashikiana katika track akdhaa ikiwemo"It's Murda" kutoka katika albam ya Ja Rule Venni Vetti Vecci ya mwaka 1999Ja Rule anasema anaamini DMX ana uwezo wa kurudi na watu kumpenda tena tu akiamua kubadilisha mtindo wa maisha na kuamua kufanya muziki.Ja nasema binadamau huwa wanatoa nafasi nyingine kwa mtu aliyekosea,ni yeye tu kuamua na kubadlika,watu watampokea na kununua kazi zake. Ja Rule hivi karibuni atatoka na simema inayokwenda kwa jina la ''
I'm in Love with a Church Girl''.
0 comments:
Post a Comment