Watoto wawili wa gwiji wa miziki,Marvin Gaye wamemshitaki Robin Thicke kwa kile walichokiita wizi wa wimbo unaofanya vizuri sana kwa sasa katika radio stesheni na club mbalimbali duniani, "Blurred Lines"
Watoto hao wawili marehemu Marvin Gaye,Nona Gaye na Frankie Christian Gaye wamefungua mashtaka jana jumatano tar 30,mashtaka ambayo wanasema Robin Thicke ameiba wimbo wa baba yao unaofahamika kwa jina la "Got to Give It Up" na kuubadilisha aina ya uimbaji.Watoto hao wamesema wana ushahidi wa kutosha kwani hata Robin Thicke mwenyewe alikili katika mahojiano na mtandao wa Billboard kwamba alikuwa mshabiki mkubwa sana wa Marving Gaye na maranyingi husikiliza nyimbo zake.
Watoto hao wawili marehemu Marvin Gaye,Nona Gaye na Frankie Christian Gaye pia wamesema hata wimbo wa Robin "Love After War" ni kopy ya wimbo wa marehemu baba yao Marvin,"After the Dance."
Nona na Frankie Gaye wanata walipwe sehemu ya faida iliyopatikana kutokana na nyimbo hizo haswa "Blurred Lines" ambayo imekaa namba moja kwa chati za Billboard kwa takribani wiki 12.
Thursday, October 31, 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment