Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Thursday, November 21, 2013

112013_chris_brown_court_launch
Chris Brown ameamriwa kungia tena rehab kwaajili ya ya kujifunza kuzikabili hasira na mara hii ni siku 90. 
Brown alikutana na maamuzi hayo pale alipohudhuria mahakamani jana jumatanao tar 20 nov kwaajili ya kusikiliza muendelezo wa kesi ya kumpiga aliyekuwa girlfriend wake,Rihanna.
Jaji amempa Brown adhabu ya kifungo cha nyumbani cha miezi mitatu,kufanya shughuli za kijamii kwa masaa 24 kila wiki na amemtaka apatiwe vipimo vya madawa ya kulevya.
Hapo awali Brown alienda rehabu kwa wiki mbili huko Malibu rehab facility for anger management  kwaajili ya ya kujifunza kuzikabili hasira,lakini alifanya kosa lingine pale alipovunja kioo cha gari ya mama yake kwa kurusha jiwe.
Mtandao wa TMZ unaripoti kwamba mama yake Brown alikuwa akimtaka Brown aendelee na mafunzo hayo kwa muda zaidi ndipo ubishani ulipoanza mpaka kupelekea kurusha kitu kinachosemekana jiwe lililovunja kioo cha gari ya mama yake.
Brown anatakiwa tena mahakamani Dec 16.

0 comments:

Post a Comment