Hivi karibuni tulitaarifiwa mimbaji mahiri wa muziki wa r&b na pop,Chris Brown aliingia rehab kwaajili ya kupata msaada wa kuzikabili hasira baada ya tukio la wikiendi iliyopita la kushambulia mtu huko Washington Dc.
Maafisa wa masuala ya uangalizi wa kisheria (probation) wametoa tamko kufuatia yukio hilo na hatua aliyochukua Chriss Brown ya kujipeleka rehab.Wakiongea na chanzi kimoja cha habari hizi maafisa hao wamesema,Chris Brown kwenda rehab haiwezi kuwabadilisha na wala haiwezi kumsaidia kumuepusha na kikombe cha adhabu kinachomsubiri ikiwa atakutwa na kosa moja kwa moja.Inasemekana adhabu inayomnyemelea Chriss Brown ikiwa atakiuka masharti hayo ya kutoshiriki vurugu yeyote iliyotokana na kesi ya kumpiga alikuwa mpenzi wake,Rihanna.
Friday, November 1, 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment