DMX hivi karibuni imeripotiwa yupo katika hali mbaya kifedha,akiongea na mtandao wa TMZ rappa huyo amesema anakubali yupo katika wakati mgumu tatizo analosema limesababishwa na mkewe.
Rappa DMX anamlaumu mke wake huyo kwa kuwa anapenda makuu na mambo ya kifaharikufikia kung'ang'ana kuishi katika nyumba asiyomudu kulipa kodi.
DMX alikuwa anaisi katika mjengo wa kifahari huko Mt. Kisco,New York miaka ya 2005 lakini baadaye katika miaka ya 2008 akaondoka na kumuacha mkewe Tashera japo imesajiliwa kwa jina la DMX.
DMX anakili alihama kwaajili ya kupunguza gharama za maisha lakini mkewe,Tashera alisema haondoki na atamudu gharama zote zikiwemo kulipa kodi ambayo hajlipa tangu mwaka 2008.
DMX pia amesema wakati akiwa jela,Tashera alienda benki na kuchukua kiasi cha dola 100,000 bila kumjulisha na hajui alitumia vp.
Tuesday, February 25, 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment