Akiongea katika kipindi cha The Arsenio Hall Show jana (February 18),aliyekuwa mmiliki wa studio ya Death Row Records,Suge Knight amesema kiwanda cha muziki cha marekani badokinawadhulumu wasanii kwani jasho wanalotoa ni tofauti na marejesho katika kuyathibitisha hayo alitoa mfano kwa kuwataja ma rappa anaotoka nao jimbo moja upande wa west Coast,Game na Kendrick Lamar.
Suge Knight ameongeza kusema anachoona wanachofaidika wasanii hao kuzidishiwa umaarufu na kutangazwa zaidi si kuboreshewa vipato sababu wanakatwa sana.Amesema wasanii wengi wanafurahia kumilikiwa na record label kubwa kama interscope japo wanaenda kuwa watumwa na kukamuliwa.Interscope chini yakekuna Aftermath kuna G-Unit wote hawa wakatwe na wao wakukate wewe na bado msanii ahusike na makato ya kodi ya mapato,huu nauita utumwa.
Thursday, February 20, 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment