Chicago rapper ambaye pia ni binamu wa Chief Keef,Mario Hess aka Blood Money,imeripotiwa ameuwawa kwarisasi kitaani kwao huko Chicago ikiwa ni wiki kadhaa tangu apate dili la kuwa chini ya record label kubwa ya Interscope Records.Ripoti zaidi zinadai tukio hilo limetokea siku ya jumatani usiku (April 9).
Manager wa msanii huyo ambaye ni binamu yake pia,Renaldo Reuben Hess akiongea a waandishi wa habri amesema,kuachana na maisha ya mitaani na kufanya kazi na record label kubwa ilikuwa ni ndoto ya Mario Hess aka Blood Money na alikuwa anikamilisha lakini kwa bahati mbaya umauti umemkuta.Polisi wanasema Mario Hess,mwenye umri wa miaka 33 aliuwawa kwa kuigwa risasi kama 10 mida ya saa tatu na nusu usiku maeneo ya 5600 block South Elizabeth Street akiwa jiani kuelekea studio.Sambaba na Mario Hess aka Blood Money alikuwapo pia ndugu yake ambaye naye aliumizwa vibaya na risasi na kukimbizwa katika hospitali ya John H. Stroger, Jr. Hospital .
0 comments:
Post a Comment