Mtandao wa BBC.com inaripoti Polisi nchini Uhispania, wanasema wamemkamata shabiki
aliyemtupia mchezaji soka wa Barcelona Dani Alves Ndizi siku ya
Jumapili akiwa uwanjani.
Dani ni raia wa Brazil anayesakatia soka yake katika klabu ya Barcelona.Alves alichukua Ndizi hiyo na kuila, kitendo ambacho kimemletea sifa duniani kote na hata kuanzisha kampeini dhidi ya ubaguzi wa rangi katika mitandao ya kijamii.
Shabiki huyo aliyekamatwa anajulikana kama David Campaya na ana umri wa miaka 26 anayeunga mkono klabu ya Villarreal.
Klabu hiyo ilisema kwamba mwanamume huyo hataruhusiwa tena kuhudhuria mechi zozote msimu huu na kwamba amepigwa marufuku maisha.
Mchezaji huyo alisema alishangazwa sana na uungwaji mkono aliopata kutoka kote duniani watu wengi wakionekana kwenye mitandao ya kijamii wakila Ndizi kama ishara ya kumuunga mkono Alves.
0 comments:
Post a Comment