Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Thursday, June 26, 2014

Michael Jackson and Beyoncé
Michael Joseph Jackson (29 Agosti 1958) alikuwa mwimbaji, dansa na mburudishaji kutoka nchini Marekani. Hufahamika zaidi kwa jina la kiheshima-utani kama Mfalme wa Pop. Hutambulika kama mburudishaji aliyepata mafanikio zaidi kwa muda wote, na moja kati ya waburudishaji wenye mvuto na athira kubwa katika medani ya muziki. Michango yake katika muziki, dansi na fasheni, na hasa suala la kuanika hadharani maisha yake binafsi, imemfanya awe kioo cha ulimwengu katika tamaduni maarufu kwa ziaidi ya miongo minne .
Akiwa pamoja na ndugu zake, Jackson amefanya uongozi wa uimbaji kwa mara ya kwanza akiwa kama mwanachama mdogo kabisa katika kundi la The Jackson 5 mnamo mwaka wa 1964. Ameanza kazi ya usanii wa kujitegemea kunako mwaka wa 1971. Albamu yake ya mwaka wa 1982 Thriller imebaki kuwa albamu yenye mauzo bora kwa muda wote. Mchango waka katika utengenezaji wa muziki wa video umeinua kutoka katika hali ya kawaida hadi katika hali ya kisanii zaidi: video zake kama vile Billie Jean, Beat It na Thriller inamfanya kuwa msanii Mmarekani Mweusi wa kwanza kupata kupigiwa nyimbo yake sana kwenye MTV. Jackson ameipa umaarufu baadhi ya maunja ya kudansi, kama vile robot na moonwalk. Staili ya muziki wake, staili ya sauti yake na zile koregrafia zilitambulika vizazi kwa vizazi, kirangi na hata katika mipaka ya kitamaduni.
Jackson ni mmoja kati ya wasanii wachache waliowekwa mara mbili kwenye Rock and Roll Hall of Fame. Mafanikio mengine yanajumlisha Guinness World Records (ikiwa ni pamoja Mburudishaji Mwenye Mafanikio kwa Muda Wote), Tuzo za Grammy 15 (ikiwa ni pamoja na ile ya Living Legend Award na ile ya Lifetime Achievement Award), 26 American Music Awards (24 akiwa kama msanii pekee ya kujitegemea, ikiwa ni pamoja na moja kwa ajili ya Msanii wa Karne)—zaidi ya msanii mwingine yeyote— single zake 17 zimeshika nafasi ya kwanza huko nchini Marekani (ikiwa ni pamoja na nne akiwa kama mwanachama wa kina Jackson 5), na inakadiriwa kafanya mauzo ya rekodi zaidi ya milioni 750 dunia nzima, inafanya kuwa miongoni mwa wasanii waliouza rekodi zao vilivyo kwa muda wote na haijawahi kutokea .
Michael Jackson amefariki mnamo tar. 25 Juni 2009 baada ya kuwaishwa katika hospitali ya UCLA Medical Center. Ilifikiriwa kwamba alipata mshtuko wa moyo, ikiwa na maana kwamba moyo wake ulisimama na imeonekana ya kwamba sababu yake ilikuwa matumizi mabaya ya madawa mengi mno.At 4:36 pm local time, the Los Angeles coroner confirmed Jackson's death.
Wakati wa umauti wake, Jackson alikuwa na umri wa miaka 50. Tetesi za habari za kifo cha Jackson, kimevunja rekodi ya mtandao na kusababisha msongamano mtandaoni kwa kuwapa tabu Google, Twitter, Facebook, na Yahoo msongamano mkubwa wa utafutaji wa habari zake
Akimkumbuka na kumshukuru Michael Jackson Beyonce alisema: “Michael Jackson changed me, and helped me to become the artist I am thank you Michael,”

0 comments:

Post a Comment