Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Wednesday, June 25, 2014

 
FIFA imeatangaza kuanza kumchunguza striker wa timu ya Liverpoll inayoshiriki lihi kuu ya uingereza na timu ya taifa ya UruguayLuis Suarez, kwa kumng'ata begani beki wa Italy,Giorgio Chiellini siku ya jana june 24 wakati timu zao zilipokutana katika katika kombe la dunia katika hatua ya mtoano ambapo Uruguay walitoka kifua mbele kwa kulaza Italy 1-0.
Fifa imesema wametoa muda hadi leo saa 3 usiku kwa timu ya taifa ya Uruguay kutoa utetezi na ufafanuzi  juu ya tukio la Suarez kumng'ata begani beki wa Italy,Giorgio Chiellini ambapo iwapo atakutwa na makosa ya makusudi anaweza kukumbwa na adhabu ndogo ya kutocheza mechi 2 ama kungiwa miaka miwili.
Uruguay' imeingia katika 16 bora na itavaana na Colombia siku ya jumamosi June 28.
Suarez alishafungiwa kucheza mechi 7 kwa tukio la kumng'ata mtu mwaka 2010. Na mwaka 2013alifungiwa mechi 10 na English FA kwa kumng'ata mchezaji wa Chelsea,Branislav Ivanovic. 
Kufuatia tukio hilo mchezaji wa Manchester United Patrice Evra amesema atafurahi kuona FIFA wakimpa adfhabu kubwa kuliko za mwanzo.
Naye mchezaji beki wa Italy, Chiellini , amesema “Suarez ni nyoka na ajachukuliwa hatua jana kwasababu  FIFA wanapendelea mastar wao wacheze kombe la dunia. 
Wapenzi wa soka wamempa cheo cha dhihaka Suarez kwa kusema ukiachilia mbali upachikaji wake wa magoli pia ana hat trick ya kung'ata.
Tazama hapo chini picha za matukio mbali mbali ya Suarez kung'ata.

  

0 comments:

Post a Comment