Mwanamke aliyehukumiwa kifo nchini Sudan kwa kuasi dini ameachiliwa huru.
Wakili wake Elshareef Ali, ameambia BBC kuwa mwanamke huyo aliyekiuka dini kwa kuolewa na mwanamume mkristo aliachiliwa huru Jumatatu.
Meriam ameolewa na mwanamume mkristo na alihukumiwa kifo na mahakama ya kiisilamu kwa kosa la kuasi dini, baada ya kukata kukana kuwa yeye ni mkristo.Hukumu ya kifo iliyotolewa dhidi ya Meriam Ibrahim,ilibatilishwa na mahakama ya rufaa, kwa mujibu wa shirika la habari la Sudan Suna.
Hukumu dhidi yake ilichochea viongozi wa kimataifa walioilaani wakisema inakiuka haki za binadamu.
Mumewe Meriam Daniel Wani, alisema kuwa ana hamu sana kumuona mkewe kwani taarifa hiyo ilitolewa bila yeye mwenyewe kuitarajia.
Ameambia BBC kuwa anataka familia yake kuondoka nchini Sudan haraka iwezekanavyo.
Wanandoa hao waliona kanisanmi baada ya kukutana mwaka 2011.
Hukumu ya kifo dhidi ya Meriam Yahia Ibrahim Ishag, ambaye alijifungulia gerezani, ilisababisha gadhabu sana hadi katika ulingo wa kimataifa.
"Tuna furaha sana kuhusu hatua hii ya serikalli na tunaelekea sasa kumchukua,'' alisema wakili wa Bi Meriam Elshareef Ali.
Bwana Ali alisema kuwa Bi Meriam alionyesha ujasiri mkubwa sana wakati huu wa masaibu yaliyomkumba.
0 comments:
Post a Comment