Mabao ya muda wa ziada ya Kevin de Bruyne na mchezaji wa akiba Romelu Lukaku yaliwezesha Ubeljiji kutinga hatua ya robo fainali ya kombe la dunia timu hiyo ilipoilaza Marekani mabao 2-1 huku Salvador Brazil.
Hii ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kwa Ubeljiji kufuzu kwa hatua hiyo ya robo fainali baada ya kipindi cha miaka 28 .
Tineja mshambulizi wa Lille mzaliwa wa Kenya Divock Origi alianza katika mechi hii badala yake Lukaku na alichangia katika mashambulizi ya lango la Marekani kwa ushirikiano na Jan Vertonghen na De Bruyne.Kipa wa marekani Tim Howard alitajwa kuwa mchezaji bora katika mechi hiyo kufuatia mchezo mzuri aliodhihirisha kwa kuokoa mikwaju tele kutoka kwa vijana wa Marc Wilmots .
0 comments:
Post a Comment