Mwanamitindo na mwanamuziki mmoja wa Kikorea,Hang Mioku (50) y ambaye alipenda sana kufanyiwa upasuaji wa kutengeneza sura hivi karibuni ameripotiwa kujiharibu vibaya sura yake baada ya kutumia kemikali kwa kujipimia mwenyewe.
Gazeti la International Business Times limeandika,Mwanamitindo na mwanamuziki huyo wa wa Kikorea baada ya kufanyiwa upasuaji mara nyingi,aliwaendea tena madaktari apasuliwe tena na kukataliwa na ndipo alipoamua kujitibu kwa kujidunga usoni na kemikali mbalimbali na mafuta ya kula
Hang Mioku,amejiharibu sana uso wake baada ya kujidunga kemikali hizo na kuifany kuumuka kuvimba na kuwa mbaya.
Mioku mwenye umri wa miaka 50 alianza kufanyiwa upasuaji tangu akiwa na umri wa miaka 28 na kujiona mzuri kisha akahamia Japan.
0 comments:
Post a Comment