Mwaka wa 2015 utakuwa mwaka wa kazi kwa muimbaji mahiri Chris Brown ukiachana na muziki ambayo ndiyo kazi yake amepewa kazi nyingine na mahakama.
Chris jana alihudhuria mahakamani kusikiliza kesi yake inayomkabili ya kumpiga aliyekuwa mpenzi wake, Rihanna mwaka 2009.Muda wake wa kufanya kazi za kijamii umeongezwa na kufikia siku 4 kwa wiki kazi ambayo huifanya kwa takribani masaa 8 kwa siki,na anatakiwa kumaliza adhabu hiyo mapema January 2015.
Chris pamoja na kuwa na kesi hiyo amekuwa matatani kisheria kwa makosa mengine mbali mbali yakiwemo ya kuvunja sheria iliyomuweka chini ya uangalizi ya mwendo kasi tofauti na vielekezi vya barabarani.
Dakitari anayemtibu Chris ameandika barua kwa hakimu kuangalia upya ratiba hiyo kwani mteja wake ana ratiba ya matibabu pia ambayo itaingiliana na adhabu hiyo.
0 comments:
Post a Comment