Swali kubwa kwa wengi ni je,Miley anatoka kimapenzi na mtoto wa muigizaji nguli wa filamu Hollywood, Arnold?
Miley Cyrus anapenda kupamba vichwa vya habari ila hili la kuhusishwa kimapenzi na mtoto wa Anold Schwarnegger kama ameliweka siri japo ni wazi kwamba ameahana na laiyekuwa mpenzi wake, Liam Hemsworth, mwaka jana.
Muimbaji huoy wa The "Wrecking Ball" amepigwa picha akila bata na katika sikukuu ya Haloween na mtoto wa Arnold Schwarzenegger mwenye umri wa miaka 21 Patrck ambaye ni amwanafunzi katika chuo cha USC na ni mwanamitindo
Wakati wawili hao wakionekana kufurahia ukaribu wao,mambo si shwari upande wa pili japo imezoeleka kuwa ni furaha pale wanapochipua wapenzi wapya huko Hollywood.Taarifa toka kwa mtu wa karibu na wazazi na ndugu wa karibu wa Patrick ambao ni sambamba na mama yake,Maria Shriver ambaye ni biamu wa John F. Kennedy,hajafurahishwa na amechukizwa na habari hizo.
Habari zaidi zimesema familia ya Patrick imejaribu kuongea naye kuhusu kuacha ukaribu na Miley wakihofia mwanamuziki huyo anaweza kuiletea sifa mbaya familia hiyo yenye heshima Hollywood.
Patrick si mgeni na mambo haya kwani ameigiza katika video ya Ariana Grande ya wimbo “Right There,”
Patrick si mgeni na mambo haya kwani ameigiza katika video ya Ariana Grande ya wimbo “Right There,”
Wapiga picha waliomuona Miley ambaye anatiiza miaka 22 mwezi huu akitoka katika nyumba ya Patrick huko Los Angeles siku ya ijumaa.
0 comments:
Post a Comment