The R&B superstar Chris Brown ameingia matatani baada ya kuvunja sheria na kukiuka taratibu za majaribio katika kesi inayomuhusu aliyekuwa mpenzi wake,Rihanna.Moakosa aliyoyafanya Brown ni pamoja na kusafiri kwaajili ya kwenda kutumbiza katika Concert bila ruhusa ya mahakama na kutokamilisha adhabu ya kazi za kijamii kwa wakati.
Chris Brown jana siku ya alhamis tarehe 15 Jan alihudhuria mahakamani huko L.A kusikiliza muendelezo wa kesi inayomkabili ya kumpiga aliyekuwa mpenzi wake,Rihanna mwaka 2009.Muendesha mashtaka alimsomea mashtaka R&B star huyo kwa kosa la kwenda kutumbuiza huko San Jose bila kibali maalumu cha mahakama.Brown pia alitakiwa kufanya kazi za kijamii ambapo alitakiwa kukamilisha masaa 1000 ifikapo mwezi Jan lakini alifanya masaa 200 tu.
Brown pia anashukiwa kwa vitendo viovu kwani mwezi August mwaka 2014 alipokuwa akitumbuiza jukwaani katika pati aliyoiandaa huko West Hollywood lilitokea shambulizi la risasi lililopelekea mdau wa Hiphop Suge Knight kuumizwa.
Brown pia ametajwa katika tukio lingine lililotokea jumapili iliyopita katika kilabu kimoja huko San Jose alipokuwa akitumbuiza ikatokea vurugu kubwa baada ya kusikika milio ya risasi iliyopelkea watu watano kujeruhiwa kwa risasi.
0 comments:
Post a Comment