Aaliyah angekuwa anatimiza miaka 36 leo Jan. 16.
Aaliyah alitunukiwa u Princess wa R&B akiwa na umri wa miaka 22 tu na alishaingia katika kuwania tuzo kubwa duniani za Grammy.Muimbaji huyu alifariki August 25, 2001,huko Marsh Harbour, Bahamas katika ajali mbaya ya ndege.
Helen Folasade Adu (amezaliwa 16 Januari 1959) ni mwanamuziki kutoka nchi ya Nigeria. Anajulikana zaidi kwa jina la Sade. Sade ambaye amewahi kupata Tuzo ya Grammy hasa ni mwimbaji na mtunzi.
Sade alizaliwa katika mji wa Ibadan katika Jimbo la Oyo. Baba yake, Bisi Adu, alikuwa ni Mnigeria, mhadhiri wa masuala ya uchumi, na mama yake, Anne Hayes, alikuwa ni nesi toka Uingereza. Baada ya baba na mama yake kuachana, mama yake alirudi Uingereza ambapo aliwachukua Sade na kaka yake, Banji. Akiwa Uingereza, Sade alijenga mapenzi na masuala ya mitindo, dansi, na kuimba. Wakati huo alipenda kuwasikiliza wanamuziki kama Marvin Gaye, Curtis Mayfield, na Donny Hathaway.
0 comments:
Post a Comment