Msanii wa muziki wa rap nchini
Marekani,Lil Wayne katika kitabu alichoandika amesema alikuwa tayari
kumshambulia msanii mwenza ambaye pia ni rafiki yake,Drake kwa kile
alichosema kwamba rafiki yake huyo alimwendea kinyume na mpenzi
wake.Mtandao wa kidaku wa TMZ wa nchini Marekani,ulipata taarifa ya
mapendekezo ya kitabu hicho ambayo yametumwa kwa wachapishaji kadhaa.
Wayne anadai kwamba wakati alipokuwa akihudumia kifungo chake jela
katika kisiwa cha Rakers kwa kumiliki bunduki bila kibali,inadaiwa kuwa
Drake alimtembelea na kukiri mbele yake kwamba ali lala na mpenziwe.Lil
Wayne alisema :Hiki ni kitendo ambacho mwanamume ambaye yuko jela
hapendi kusikia kwa sababu ni mungu anayejua ni nini ningelifanya iwapo
ningekuwa nje.
Wayne alikiri katika mapendekezo hayo kwamba yeye
na mpenziwe walikuwa wakigombana sana ndipo Drake akamwambia kwamba
alilala naye.Hatahivyo Wayne anasema kuwa mwanamke huyo alimwambia
kwamba alifanya mapenzi na Drake siku moja kabla ya kukutana na Wayne.
Saturday, March 21, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment