Mahusiano yao unaweza kusema yalivunjika miaka kadhaa sasa laikini muimbaji mahiri Chris Brown, 26,bado anadai nafasi ya Rihanna, 27 bado ipo katika moyo wake.Akihojiwa na mtangazi Tim Westwood,Breezy amesema si tu kwamba yeye na Rihanna wapo poa na wanajuliana hali bali bado kila mmoja ana mapenzi ya kweli kwa mwenzake,bado tunapendana.Chris Browm katika mahojiano hayo aliongeza kusema pengine kinachowaunganisha ni history kwani wamejuana tangu wakiwa wadogo umri wa miaka 14/15 na wamekuwa wakiungana mkono katika kazi zao hata hivi karibuni Rihanna alihudhuria sehemu ya mazoezi ya Chris Brown alipokuwa katika maandalizi ya kutumbuiza katika sherehe za tuzo za BET 2015.
0 comments:
Post a Comment