Rapa Tyga alilipwa kiasi cha dola 25,000 na alisaini mkataba na promota mmoja kwamba moja kati ya masharti ni kutotumbuiza kwa wiki moja kabla karibu na eneo litapofanyika tamasha aliloandaa.
Promota huyo anadai rapa Tyga alipanda jukwaani usiku siku moja kabla katika club moja iliyopo karibu na club aliyotakiwa kutumbiza kitu kilichopelekea watu kutokuja kwa wingi katika tamasha aliloandaa ambalo lilifanyika siku inafuata baada ya Tyga kuonekana jukwaani katika Club ya jirani.Promota huyo aliyemlipa Tyga do 25,000 amemtaka rappa huyo kumlipa fidia ya dol 100,000 kutokana na uharibifu aliousababisha.
0 comments:
Post a Comment