Romy Jones aalialika mastaa kibao akiwa ndugu yake,Diamond Platnums, na masta kibao kama Shilole,Nuh Mziwanda,Barnaba Classic,Jux,Vanessa Mdee,T.I,D,Q Chilla,Domokaya na mastaa wa fani mbali mbali wakiwamo madj kama Dj Zero wa Clouds,Dj Tas wa Magic Fm,Dj Ommy Crazy wa East Africa Fm,Dj Nicotrack,Dj Omy wa Maisha Club.
Sherehe hiyo ilijaa mbwembwe na burudani za hapa na pale kwani ukuachilia mbali burudani safi ya muziki pia wasanii wa muziki wa kizazi kipya walitumbuiza.Mbali na kutumbuiza,Diamond platnum alichukua nafasi hiyo kuwapaisha na kwashukuru wasanii waliomtangulia kwa kumfanya awe pale alipo.Sambamba na wengi aliowataja,Diamond aliwaongelea T.I.D na Q Chila kwanza aliwapongeza kitendo chao cha kumaliza tofauti zao na pia aliwataja kuwa wana mchango mkubwa sana kwake huku akimtaja Q Chila katika uimbaji na T.I.D katika kuvaa,kucheza na kushambulia jukwaa.
0 comments:
Post a Comment