Rapa mmoja chipukizi aliyetambulika kwa jina la
J.Luchiano amejikuta matatani badala ya kutimiza ndoto zake.
J.Luchiano alitaka kutimiza ndoto zake kwa kumsikilizisha bosi wa MMG,Rick Ross kazi zake kwa kumuachia asikilize mixtape yake lakini kwa bahati mbaya alijikuta akitumia njia sizo na kuingia matatani.Luchiano aliruka geti laRick Ross na kujipiga selfies kadhaa katika eneo la mjengo wa Ross na kuacha mixtape yake na kisha kutupia picha hizo mitandaoni.Tukio hilo limempelekea kijana huyo kujikuta mikononi mwa polisi baada ya kutegwa na wanasheria waRoss kama kazi yake imekubaliwa hivyo aje ofisini waongee ndipo J alipowahi fasta na kukaribishw ana glass ya maji akisubiri waongee na badala yake wakaingia polisi na kumtia pingu kwa kosa la kuingia eneo la mtu bila ruhusa.
0 comments:
Post a Comment