Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Thursday, November 24, 2016


Beyoncé na mumewe Jay Z  wamekamilisha iliyokuwa minong'no ya tangu mwezi Feb kwamba wanahamia Los Angeles.
Beyoncé na mumewe Jay Z ni kweli wamehama pwani ya mashariki,New York na kuhamia pwani ya magharibi L.A  ambapo sababu kubwa imetajwa ni kuwa karibu na shule maalumu ya binti yao Blue Ivy. 
Mtu wa karibu na Beyoncé na mumewe Jay Z  amesema mastaa hao wanalipa ada dola 19,000 kwa mwaka kwaajili ya program maalumu atakayosomea binti yao sambamba na baadhi ya mahitaji.
Jay Z (ambaye ni mzaliwa wa Brooklyn) na Bey ambaye ni mzaliwa wa Houston wamehamia L.A  lakini bado wanamiliki mjengo wao wa kifahari uliopo New York City's Tribeca neighborhood.
Taariza ndani zainasema Beyoncé na mumewe Jay Z wanashirikiana kwa karibu kimalezi haswa katika mambo ya shule ya binti yao Blue ambapo wamegawana jukumu la kumpeleka na kumchukua na kuhudhuria vikao vya wazazi na walimu.

0 comments:

Post a Comment