Rapa Lil Wayneaameshindwa kutumbuiza katika onyesho lililotakiwa kufanyika huko Columbia, South Carolina concert weekend hii.
Weezy ambaye ndiye aliyekuwa kinara katika onyesho hilo alianzisha utata pale alipogoma kupita mahala maalumu pa ukaguzi kwa yeye na watu wake ndipo uongozi wa juu wa ukumbi huo walipoamua kutoa muongozo kwamba kama Weezy hataki kukaguliwa asiingie ukumbini kwa kile walichokidai usalama wa wafanyakazi wao na maelfu ya mashabiki waliohudhuria.
Onyesho liliendelea bila Lil Wayne na 2 Chainz, ila rapa wa kike Cardi B na muimbaji Tory Lanez walifungua show kama ilivypangwa.
Wayne na camp yake hawajasema lolote japo kuna tangazo liltolewa na waandaji kwamba kuna kiasi kitarejeshwa kwa mashabiki walionunua tiketi.
Monday, October 2, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment