Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Friday, May 16, 2014

 0512-jay-z-solange-tmz-01
Bbc.co,uk imeandika,Mfanyakazi aliyefichua kanda iliyoleta gumzo inayomuonyesha mwanamuziki Jay Z akishambuliwa na shemeji yake,Solange amefukuzwa kazi.
vurumai kati ya Jay Z na shemeji yake,Solange Knowles zilinaswa na Kamera ya lifti ikionyesh Solange akimshambulia Jay Z,ingawa haijulikani kilichosababisha vita hivyo.
Kanda hiyo ya video ambayo ilitolewa kwanza kwenye tovuti ya udaku kuhusu watu maarufu TMZ,ilimwonyesha dadake Beyonce akimpiga Jay Z baada ya tamsha la Met mjini Los Angeles, iliyofanyika mwezi Mei tarehe 5.
Baada ya ugomvi mkali baina yao,mlinzi aliingilia kati. Hata hivyo kanda hiyo haikuwa na sauti.
Hoteli hiyo inayojulikana kama ‘The Standard ilisema kuwa ilishtushwa sana na kufichuliwa kwa matukio ya Lifti na ikamtaja mfanyakazi huyo aliyehusika katika ufichuzi huo.
Mfanyikazi huyo alifutwa kazi kwa kosa la kuvunja sheria za usalama kwa kufichua video za CCTV, ambazo ni za siri.
Hoteli hiyo iliongeza kuwa ingetoa habari zingine zote za ziada kwa idara ya kupambana na wakiukaji wa sheria.

0 comments:

Post a Comment