Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Thursday, May 15, 2014

 
Mtandao wa.bbc.co.uk/swahili umeandika,mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja amenusurika kifo baada ya kuanguka kutoka orofa ya 11 ya jengo moja mjini Minnesota Marekani.
Vyombo vya habari katika jimbo hilo vimeripoti kuwa Musa Dayib, amevunjika mkono mara mbili na kwa sasa anapumua kwa usaidizi wa mashine japo madaktari wanamtarajia kuishi.

Musa aliteleza katikati ya mianya inayozingira sebule yao katika orofa ya 11 ya mjengo huo wenye nyumba na makazi ya watu.Muuguzi mkuu katika zahanati aliyolazwa amesema kuwa Musa anatarajiwa kuishi baada ya kuanguka katika eneo lisilo kavu sana.
Jamaa na marafiki wa familia hiyo ya kisomali wamepigwa na butwaa kutokana na tukio hilo.
Dakta Tina Slusher, aliyemhudumia mtoto Musa, alisema hakuna vile mtu mzima angenusurika baada ya kuanguka umbali kama huo.
Bila shaka huu ni muujiza wa Mwenyezi mungu.

0 comments:

Post a Comment