bbc.co.uk/swahili/michezimeandika,Louis van Gaal ametangazwa kuwa kocha mpya wa
Manchester United, huku aliyekuwa kocha wa muda Ryan Giggs akifanywa
kuwa msaidizi wake.
Raiya huyo wa Uholanzi, ametia saini mkataba wa
miaka mitatu, na atachukua usukani wa timu hiyo baada ya kuiongoza timu
ya taifa ya Netherlands katika kombe la dunia litakalofanyika nchini
Brazil.
Mataji ya kitaifa:
Ajax (1993-94, 1994-95, 1995-96),
Barcelona (1997-98, 1998-99),
Bayern Munich (2009-10)Klabu bingwa ulaya:
Ajax (1994-95)Kombe la Uefa:
Ajax (1991-92)
Ajax (1993-94, 1994-95, 1995-96),
Barcelona (1997-98, 1998-99),
Bayern Munich (2009-10)Klabu bingwa ulaya:
Ajax (1994-95)Kombe la Uefa:
Ajax (1991-92)
Alikutana na Van Gaal nchini Netherlands juma lililopita ili kuzungumza kuhusu hatima yake katika klabu hiyo,kama mmoja kati ya wakufunzi na wakati huo huo akiwa mchezaji.
United walimaliza wa saba katika ligi ya premier, baada ya waliokuwa mabingwa watetezi kushindwa na Manchester City, Liverpool na Chelsea.
Walishindwa kufuzu kucheza mechi ya vilabu bingwa wa Uropa kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 1995-96, na hawatacheza mechi zozote za kiropa kwa ujumla kwa mara ya kwanza kwa miaka 26 iliyopita.
Mchezaji mkongwe wa klabu hiyo Giggs, meneja wa Real Madrid Carlo Ancelotti na meneja wa Borussia Dortmund Jurgen Klopp walikuwa wamehusishwa na kazi hiyo, lakini Van Gaal ndiye aliyechaguliwa ili kuiongoza timu hiyo kurejea kileleni mwa ligi za premier na michezo ya Uropa
Kocha huyo mpya anatarajiwa kupewa pesa nyingi ili kuwasajili wachezaji wapya
0 comments:
Post a Comment