Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Friday, February 27, 2015



  
Kanye West, 37, hivi karibuni alifanya mahojiano na kituo cha redio maarufu duniani BBC 1 na mtangazaji Zane Lowe.
Wakiendelea na mahojiano,Kanye West alilengwa na machozi pale alipo ulizwa kuhusu mwanamitindo anayemzimia zaidi akamtaja Profesa wa mitindo Louise Wilson aliyefariki mwezi May mwaka jana (2014) ambaye alikuwa mwalimu katika chuo cha Central Saint Martins College of Arts and Design huko London kuanzioa mwaka 1992 mpaka 2014 na wanafunzi wake ni wanamitindo maarufu duniani kama Alexander McQueen, Jonathan Saunders, Christopher Kane, Marios Schwab, Peter Jensen, Richard Nicoll, Christopher Shannon and Sophia Kokosalaki na hata rappa Kanye West.
Kanye West pia aliongea kuhusu kuomba radhi kwa muimbaji Beck kufuatia kukosoa uteuzi wake kama mshindi wa tuzo ya albamu bora katika tuzo za Grammy.Kanye West jana Feb. 26 alimuomba radhi Beck kupitia akaunti yake ya Twitter kwa kuandika:I would like to publicly apologize to Beck, I’m sorry Beck.
Pia rappa Kanye West alimuomba radhi muimbaji Bruno Mars kwa kuandika:  I also want to publicly apologize to Bruno Mars, I used to hate on him but I really respect what he does as an artist katika akaunti yake ya Twitter.
Kanye amemwomba radhi Bruno Mars na kusema alikuwa akimchukia lakini kwasasa anamuheshimu kwa yale ayafanyayo kama msanii na amemuomba ashiriki katika wimbo anaoshiriki kuuandaa na 88-Keys, Puff Daddy na amemulika Odd Future frontman Tyler the Creator kuongoza video ya wimbo huo.


0 comments:

Post a Comment