Presenter/DJ at RadioOne stay with me "Dj Show" Monday to Friday

RadioOne Dar es salaam 89.7FM|Arusha 95.3FM|Tabora 98.1FM|Dodoma 100.8FM|Mwanza 102.9FM|Moshi 132.3KHZ|Morogoro 103.2MHZ|Tanga 106.3MHZ|Bukoba 92.1MHZ Home of Good Music Tanzania

Friday, March 6, 2015

Shahidi ambaye alishuhudia ndege hiyo ndogo iliyokuwa ikiendeshwa na star wa filamu za action marekani,Harrison Ford,amesema ndege hiyo ilianguka katika kiwanja cha mchezo wa Golf huko L.A na yeye alikuwa wa kwanza kufika kwaajili ya kutoa msaada na baadaye wakaja watu wengine wawili na madokta walifika na kumpatia huduma ya kwanza na kumuondoa mtu huyo hara toka katika ndege hiyo wakihofia itawaka moto.
Shahidi huyo ameongeza kusema alimuona Harrison Ford akitokwa na damu nyingi kufuatiwa na jeraha alilolipata kichwani,sta huyo wa filamu baada ya kupatiwa huduma ya kwanza aliingizwa katika gari maalumu la kubebea wagonjwa na kupelekwa hospitalini kuendelea na matibabu.
Mtandao wa TMZ umeandika,Ford alikuwa akiendesha ndege hiyo ya kivita yenye siti mbili ( vintage 2-seater fighter plane) na kitu kikakorofisha ndipo alipoamua kutua katika uwanja wa mchezo wa Golf kukwepa kuvamia makazi ya watu.
Harrison Ford ni star wa filamu za action toka America ambaye filamu zake nyingi zimefanya vizuri katika mauzo na hata majumba ya sinema kuote dunuani,hizi ni baadhi ya filamu zake:Apocalipse Now,Extraordinary Measures,K19 The Window Maker,Star wars,Airf force one,The Expandables 3,Cow Boys vs Aliens nk.




0 comments:

Post a Comment